RUGAMBWA GIRLS’S FOUNDATION
Rugambwa Girls Foundation (RGF) is made up of willing and able former students of Rugambwa Girls’ Secondary School who believe in the power of creative collaboration for better future. We are the registered Foundation under Cap. 318 R.E 2002 of Civil Societies and our certificate is No. 5216. Our areas of interest are around building self esteem to young girls through supporting better health care, education, environmental conservation, and imparting entrepreneurship skills. We plan to raise funds and spend it directly to our programs as indicated in our work plans. Based on the fact that Rugambwa has produced many professionals working in different sectors, we hope most of our activities to be done by our members in collaboration with others partners to implement programs on the ground. What began as Aluminaes coming together to support 50 years Jubilee of Rugambwa Secondary School has grew and turned into a Foundation, that contributes to building our nation.
Home » » Mkutano Mkuu wa Pili (2) wa RGF, uliofanyika tarehe 18 Februari, 2017 katika ukumbi wa Hotel Defrance, Sinza, Dar es Salaam

Mkutano Mkuu wa Pili (2) wa RGF, uliofanyika tarehe 18 Februari, 2017 katika ukumbi wa Hotel Defrance, Sinza, Dar es Salaam

Written By RGF on Thursday, March 2, 2017 | 8:07 PM

Mkutano Mkuu wa pili (2) wa Rugambwa Girls Foundation uliofanyika katika ukumbi wa Defrance Hotel, Sinza, Dar es Salaam ulipitia maazimio yaliyowekwa kwenye Mkutano Mkuu wa kwanza (1) uliofanyika tarehe 29 Novemba, 2015 katika ukumbi wa Giraffe Hotel, Kunduchi, Dar es Salaam na kujadili mafanikio ya maazimio hayo.


Pia Mkutano Mkuu huu umejikita zaidi katika kuweka malengo ya kusaidia wanafunzi wa Shule ya Sekondari Rugambwa kimasomo na kimaendeleo. Pia Mkutano Mkuu umeweka mikakati ya kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu (walemavu wa aina zote) na pia kumsaidia mtoto wa kike aweze kujitambua na kufanikisha ndoto zake.

MAFANIKIO:

Katika mwaka wa 2016 RGF (Rugambwa Girls Foundation) imefanikiwa:

1. Mnamo tarehe 23 Januari, 2016, RGF ilifanikiwa kuitisha Mkutano uliofanyika LEADERS CLUB   ili kupeana mikakati na mbinu za kuwezesha kuisaidia Shule ya Sekondari ya Wasichana Rugambwa.

2. Katika Mkutano uliofanyika LEADERS CLUB, RGF ilifanikiwa kupata msaada wa TZS. 129,000,000/=  kutoka TEA (Tanzania Education Authority) ili kusaidia ujenzi wa miundo mbinu ya walemavu katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Rugambwa.

3. RGF ilifanikiwa kutoa msaada kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu (walemavu wa aina zote). Misaada iliyotolewa ni pamoja na madaftari, pedi kwa ajili ya kujihifadhi kipindi cha hedhi, mafuta ya ngozi, mafuta maalum ya ngozi kwa ajili ya albinism, sabuni za kufulia n.k. pia tuliwakatia BIMA ya AFYA wanafunzi wapatao 21.

4.  Pia tumejenga mahusiano mazuri na ofisi ya Afisa Elimu Mkoa wa Kagera, NHIF Kagera, TEA Dar es Salaam n.k.

5.  Tumefanikiwa kufanya vikao vya robo mwaka katika kipindi chote hicho cha miaka 2 toka tuanzishe umoja wetu na mafanikio tuliyoyapata ni pamoja tuliyoyataja hapa.

6. Uongozi wa RGF ulifanikiwa kukutana na Opportunity Education Foundation ili kuangalia uwezekano wa kuwasaidia wanafunzi wa Rugambwa kuweza kupata Mitaala au kujisomea kwa njia ya kutumia TABLET.

5.  RGF bado inatafuta mbinu zaidi za kuweza kuwasaidia wanafunzi wa Rugambwa Sekondari kielimu.

 
 
 
 


 
 
 

 
   
 
 
 
 
 
  
 
 
 
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 

 
 
 
 
 
 


 
 
 
  
 
 
 
  
 
 
 
 
 
 
  
 
  

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

0 comments :

Post a Comment